Jenerali Ulimwengu: Kinachoendelea serikalini, Tumerudi nyuma miaka 50 kwenye demokrasia

Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa lakini ukiangalia picha kubwa ni kwamba tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia. Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ulimwengu kasema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete. Ulimwengu ameendelea kwa kusema Mheshimiwa Kikwete anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali na pili kuzima matumaini ya wananchi na kuwaacha wanarandaranda ambayo inaweza kuleta machafuko baadae kama haitawezekana kutengeneza katiba ambayo itajenga mustakabali wa wananchi wa Tanzania.