From Tandale to the rest of the World, Diamond Platnumz is not done yet #theTrend

Emaanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', ni msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye mashabiki lukuki, staili yake ya kuimba mashairi makali imempatia umaarufu mkubwa. Mpaka Home ya Global TV Online, imemtilia maguu mpaka studio kwake, Free Nation, Sinza jijini Dar es Salaam. Kwa kawaida Mpaka Home hufanyika nyumbani lakini kutokana na kumkosa nyumbani kwa muda mrefu, Mpaka Home iliamua kumuibukia Nay wa Mitego usiku wa manane na kumkuta ofisini kwake iliyoko Sinza Jijini Dar. Jambo ambalo watu wengi hawalijui, ni kwamba kumbe jamaa amewekeza vya kutosha ambapo amekodi nyumba nzima maeneo ya Sinza ambapo ndani yake, kuna ofisi yake na pia kuna studio ambayo imetoa ajira kwa vijana kadhaa. Katika video hii, Nay wa Mitego anafunguka mambo mengi, ikiwa ni pamoja na ishu ya prodyuza wake, Mr Tee kumkimbia ambapo sasa anaye prodyuza mwingine, Osam. Msikilize mwenyewe... Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1