Mtanzania Benjamin alivyonyoa Nywele Marekani alafu mfukoni pesa haitoshi

Benjamin Fernandes ni Mtanzania ambaye ameingia kwenye headlines katika mitandao mbalimbali baada ya kuhitimu Masters kwenye Chuo Kikuu cha Biashara kinachotajwa kuwa Namba moja Duniani, Stanford, Marekani. Benjamin anayo hii story nyingine baada ya kukataa ofa za kufanya kazi kwenye makampuni makubwa ambayo yalikuwa tayari kumlipa hadi Tsh. 425m kwa mwaka kama angekubali kufanya kazi akiwa Marekani.