FULL VIDEO: Mbunge wa Ukonga Waitara alivyotolewa Bungeni

Kutoka Bungeni DODOMA, leo April 10, 2017 Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe alisimama kuomba kutoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge akitaka Bunge lisimamishe shughuli za kawaida na kuanza kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea nchini. Bashe amesema yeye pia ameshatumiwa ujumbe wa vitisho wakimwambia kuna watu 11 akiwemo yeye watafanyiwa vitendo vibaya popote watakapokuwa, hivyo analiomba Bunge lijadili suala hilo kwa dharula kwasababu sio sawa kukaa kimya.